Faida ya (OPEN FLOOR PLAN) katika ujenzi wa nyumba za leo
![]() |
Picha na https://www.homebuilding.co.uk |
Open floor plan ni aina ya ramani ya nyumba ambao ulenga kuunganisha matumizi ya maeneo kadhaa ndani ya Nyumba na kuyafanya yatumike kwa pamoja ndani ya chumba kimoja, kwa mfano kuwa na jiko ambalo limeungana na sehemu ya chakula ( dinning area) na pengine sehemu ya kupumzikia ( Sebule). Aina hii ya ujenzi wa nyumba za kuishi imeshika kasi mwanzoni mwa mika ya 90 na kwa sehemu fulani hapa nyumbani tanzania Imevutia walio wengi miaka ya hivi karibuni. ni dhairi kuwa nia ya aina hii ya ujenzi ni kupunguza kuta zisizo na maana ndani ya nyumba lakini pia kutengeneza madhali fulani ya tofauti ndani ya nyumba husika. zifuatazo ni baadhi ya faidi ya open plan
Faida ya OPEN Floor PLAN.
URAHISI WA MIZUNGUKO NDANI YA NYUMBA.
Hii ni kutokana na kuwa na eneo moja ndani ya nyumba lenye kazi tofauti totauti hiyo kupunguza milango, korido, na kuta zisizo na maana ndani ya Nyumba hivyo kurahisisha mzunguko wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine
INARAHISISHA MAWASILIANO NDANI YA NYUMBA. Bila kuta ni rahisi kwa mama mwenye nyumba aliye jikoni kuongea na mume wake aliye sebuleni au watoto wake walio sebuleni au sehemu ya kupatia chakula.
MATUMIZI YA MWANGA YA PAMOJA
Maeneo ambayo yalikuwa hayawezi kupata mwanga wa jua kutokana na kutokuwa na madirisha mfumo huu unayawezesha kupata kutokana na kutokuwa na kuta.
- INAONGEZA GHARAMA ZA NYUMBA PALE UTAKAPOTAKA KUUZA/KUPANGISHA.
Kwa maneno mepesi kabisa kama nyumba yako itakuwa imejengwa vizuri kama inavyotakiwa gharama ya nyumba yako pale utakapo amua kuua au hata kupangisha itakuwa ya kuridhisha kutokana na kuwa mfumo huu kwa sehemu fulani ndo habari ya mjini.
NI RAHISI KUANGALIA WATOTO.
Faida nyingi kubwa ya nyumba zenye open plan ni urahisi wa wazazi na walezi kuwaangali watoto wakiwa sebule au hata wakati wanakula hivyo kurahisisha usimamizi bora wa makuzi ya watoto
URAHISI WA MATUMIZI.
Kwa hakika bila kuta kwenye maeneo ya dinning au Sebule ni rahisi kufanya mipangilio tofauti tofauti wa vitu ndani ya eneo usika kutokana na matakwa yako na jinsi unavyojisikia.
ENEO MOJA LINAWEZA KUFANYA KAZI NYINGI ZAIDI.
- Kwa kuwa na open kitchen eneo moja linaweza kubadilishwa utakavyo, kwa mfano unaweza kuunganisha Dinning na Sebule na kufanya ukumbi wa sherehe ndogo ndogo mfano Brithday na au kufanya eneo la burudani kwa muda kutokana na mahitaji yako..
Kupata dondoo mbali mbali za ujenzi tafadhali jiunge na kundi letu la whatsapp kwa kubofya link hii Follow this link to join my WhatsApp group: https://chat.whatsapp.com/Ca5K5QHgGD60zZvtRN6BxT au nitumie ujumbe wako kupitia 0657324306
Comments
Post a Comment