Mambo kumi ya kuzingatia kabla haujaanza ujenzi.


Mara kadhaa tumejikuta tuko njia panda mara tu baada ya kuanza ujenzi wa nyumba za ndoto zetu p. Sababu zipo nyingi sana kwanini hali inakuwa ndivyo sivyo hasa pale tunapokuwa tuna hamu kweli ya kuanza kuishi kwenye nyumba zetu au kumiliki nyumba. yafuatayo ni mambo kumi ya kuzingatia wakati tunafikiria kuanza ujenzi.

  1. Hakikisha kiwanja chako kimepimwa na kina hati kwa wale tunaoishi mijini na kwa wale wa vijijini hakikisha una hati ya kijiji ya eneo unalotaka kujenga sababu kubwa ni kuwa na uhakika wa umiliki wa eneo unalojenga kwa usalama wa uwekezaji wako lakini pia mbali na maeneo mengi yanayo pimwa na kukubalika kuwa salama kwa ujenzi yana kuwa chini ya sheria zote za mipango miji na mazingira hiyo itakusaidia kukuweka salama kisheria lakini pia na majanga mbali mbali ya kimazingira.
  2. Tafuta ushauri wa kutosha kutoka kwa watu walio kutangulia kujenga na ambao kwa sehemu fulani nyumba zao zimekuvutia hiyo inaenda sambamba na kuonana na mtaalam wa usanifu ujenzi aliye karibu na wewe, kwani yeye ni mtu pekee mwenye taaluma ya kubadilisha wazo la mtu kichwani kuhusu jengo na kulifanya kuwa kitu.
  3. Hakikisha unazifahamu gharama za ujenzi kabla haujanza kufanya ujenzi. Hii itakuwezesha kujipanga vyema kwa muda, fedha na hata kiakiri kwani kinyume na hapo unaweza kujikuta katika dimbwi la madeni na mawazo na pengine kuvunjika moyo kabisa na kupelekea kusimisha mpango wako.
  4. Chagua mafundi sahihi na kama unaweza tafuta msimamizi mzoefu wa masuala ya ujenzi ingawa kuna ghalama fulani utalipia kwa huduma hiyo hakika unaweza kuishia kuokoa pesa nyingi sana kwa kuwa na mpango unaoeleweka wa ujenzi. Msimamizi mzuri atakupatia mafundi wazuri lakini pia atabeba dhamana yote ya shughuli hiyo hivyo endapo kama kutatokea shida yoyote yeye ndo atakuwa muhusika mkuu. Faida kuu katika hili ni kuondoa gharama zisizo na umuhimu kwenye orodha ya matumizi yako.
  5. Tumia vifaa imara na vinavyotengenezwa na kampuni za uhakika, kuna usemi unasema cha bure ni gharama kwa sehemu kubwa vitu visivyo na ubora vinaweza kukuondolea raha duniani kwani mara kadhaa utajikuta unarudia kufanya kitu ulichojiaminisha umekimaliza kwa gharama nafuu. wakati kama ukipata vifaa vizuri unaweza kutoa pesa nyingi kidogo lakini vikakaa kwa muda mrefu sana hivyo ni vema ukazingatia ubora na sio gharama.
  6. kumbuka muda ni gharama. hakika kuna utofauti mkubwa sana wa matumizi ya fedha kwa kazi moja ambayo inafanyika kwa mida tofauti, kwa mfano nyumba iliyojengwa kwa miezi miwili na nyumba ya aina hiyo hiyo ikajengwa kwa miezi kumi ni lazima gharama ziwe tofauti japo kuwa mafundi ni wale wale na vifaa ni vile vile. Nyumba iliyojengwa kwa muda mfupi ni dhairi kuwa itatumia fedha kidogo ukiringanisha na ile iliyojengwa kwa muda mrefu.
  7. Hakikisha nyumba inakutumikia na sio kinyume chake, Jenga nyumba unayoweza kuimudu kuifanyia usafi, kuifanyia marekebisho. Fikiria zaidi kuwa na nyumba ambayo itakuhudumia kwa asilimia mia moja na iwe tayari kupokea mabadiliko pale inapobidi kwa mfano ukitaka kuiongeza ukubwa. Haina maana yoyote kujenga nyumba ya vyumba kumi wakati familia yako ni ya watu watatu, au kuwa na madirisha matano kwenye chumba kimoja wakati hewa inawezekana kuzunguka kwa madirisha chini ya hapo.Nafikiri ni vema ukawa kama mbuzi anayekula kwa urefu wa kamba yake vinginevyo ni matatizo na sifa zisizokuwa na maana.
  8. Fikiria kuwa na nyumba inayoweza kukuhudumia, hii namaanisha watu wenye mahitaji maalum na wazee. waswahili wanasema ujafa ujaumbika hivyo ni vema ukafikiria kuwa na nyumba inayoweza kutumiwa na watu wenye mahitaji maalum kwa mfano wanaotumia viti vya matairi  na mambo mengine yanayo usihana na hayo.
  9. Usifate mkubo kumbuka tu hakuna jipya chini ya jua, hii inamaana badala ya kuangalia fulani amejenga vipi tafadhali hakikisha nyumba yako inajengwa unavyotaka, mara kadhaa watu wanajikuta kwenye majuto mengi sana baada ya kukamirisha ujenzi na kujikuta kile walichohisi wange pendezwa nacho ni kinyume kabisa na matakwa yao na hivyo ushauri wangu ni mwepesi tu shirikisha wataalam kujenga nyumba ya wazo lako.
  10. Jipendelee uwezavyo. haina haja ya kuwa nyumba yako ya kuishi huku unahisi kuwa chumba au sebule uliyonayo haikutoshi. ni vema ukaweka vipaumbele vyako mbele, kama ni chumba kikubwa weka kikubwa kweli, kama ni vitu vya kisasa weka kweli kweli lakini zaidi ya yote fanya mambo yote ukiwa unaangalia uwezo wako kifedha.
Nini maoni yako? unaweza kuniambia mambo ambayo unahisi ni shariti yazingatiwe tofauti na haya? toa maoni yako 

Comments