Faida ya (OPEN FLOOR PLAN) katika ujenzi wa nyumba za leo

Picha na https://www.homebuilding.co.uk Open floor plan ni aina ya ramani ya nyumba ambao ulenga kuunganisha matumizi ya maeneo kadhaa ndani ya Nyumba na kuyafanya yatumike kwa pamoja ndani ya chumba kimoja, kwa mfano kuwa na jiko ambalo limeungana na sehemu ya chakula ( dinning area) na pengine sehemu ya kupumzikia ( Sebule). Aina hii ya ujenzi wa nyumba za kuishi imeshika kasi mwanzoni mwa mika ya 90 na kwa sehemu fulani hapa nyumbani tanzania Imevutia walio wengi miaka ya hivi karibuni. ni dhairi kuwa nia ya aina hii ya ujenzi ni kupunguza kuta zisizo na maana ndani ya nyumba lakini pia kutengeneza madhali fulani ya tofauti ndani ya nyumba husika. zifuatazo ni baadhi ya faidi ya open plan Faida ya OPEN Floor PLAN. URAHISI WA MIZUNGUKO NDANI YA NYUMBA . Hii ni kutokana na kuwa na eneo moja ndani ya nyumba lenye kazi tofauti totauti hiyo kupunguza milango, korido, na kuta zisizo na maana ndani ya Nyumba hivyo kurah...